Timu ya Taifa ya Zambia Chipolopolo ikiwa chini ya kocha wa mpito Patrice Beaumelle inashuka dimbani leo kukipiga dhidi ya mabingwa wa dunia mara tano Brazil kwenye mchezo wa kirafiki utakaopigwa Birds Nest Stadium.
Mabingwa hao wa zamani wa Africa watakuwa bila ya mshambuliaji Rodger Kola, Collins Mbesuma, kiungto Mukuka Mulenga na beki Davies Nkausu ambao ni majeruhi.
Pia wachezaji Nathan Sinkala, Stopilla Sunzu, Rainford Kalaba wameshindwa kuripoti kwa wakati kwenye maandalizi ya mchezo huo.
Lakini kocha Beaumelle anaamini atachezesha kikosi imara na inawezekana akaamua kuwaanzisha wachezaji wanaocheza ligi ya nyumbani Bronson Chama, Kondwani Mtonga na Bruce Musakanya ambao watachanganywa na wazoefu Hichani Himonde, Kampamba Chintu na Joseph Musonda lakini pia inawezekana wakacheza Jimmy Chisenga au Emmanuel Mbola.
Nahodha Christopher Katongo, Noah Chivuta, Chisamba Lungu na Fwayo Tembo wapo kamili kuitumikia Zambia kwenye mchezo huo amba Jacob Mulenga kuongoza mashambulizi na James Chamanga huku Emmanuel Mayuka likiwa ni chaguo lingine.
Brazil kwa upande wao watakuwa bila ya kipa Julio Cesar,beki Thiago Silva na mshambuliaji Fred.
Felipe Luiz Scolari anatarajia kufanya mabadiliko kadhaa Diego Cavalieri atambadili Jefferson langoni wakati Daniel Alves, Dedé, David Luiz na Maxwell watatengeneza ukuta.
Lucas Leiva , Paulinho na Ramires wanatarajiwa kuanza kwen ye kiungo huku Lucas , Alexandre Pato na Jo wakiwa kwenye ushambuliaji.
Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.