Monday, October 7, 2013
EXCLUSIVE : Kocha wa timu kubwa bongo aacha kufundisha aenda kusaka ushindi kwa sangoma Morogoro
Haya yanaweza kuwa maajabu lakini kibongo bongo ndio mwendo na watu wanaona poa tu kikubwa ushindi kwa timu.
Sasa sikia hii,Kocha msaidizi wa moja ya timu kubwa hapa nchini aliamua kuiacha timu ikiwa kambini na kuamua kwenda kumsaka sangoma wa kuwapa ushindi kwenye mechi zao wanazocheza za ligi kuu.
Kocha huyo alilazimika kufunga safari kwenda Morogoro kumsaka sangoma huyo wa kuwasaidia kwenye mechi zao za ligi huku akimsifia vya kutosha mtaalamu huyo kuwa ni mkali na anaweza kuwapa mafanikio.
Kocha huyo akatia timu Morogoro akampa kazi Sangoma ya kuwapa ushindi katika mechi zao na kazi ikaanza,mechi iliyofuata wakashinda kwa mabao 2-0 dhidi ya moja ya timu ambazo zimekuwa zikitoa upinzani kwenye ligi na inafundishwa na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania,timu ambayo katika msimu uliopita iliwanyanyasa kwenye michezo yote miwili waliyokutana kwa kuwatembezea kichapo.
Baada ya mchezo huo kocha huyo akatamba kuwa Sangoma wake kafanya kazi kubwa na wamepata ushindi katika mchezo mgumu na katika mchezo uliofuata timu hiyo yenye wachezaji waliosajiliwa kwa pesa nyingi ikapata ushindi mwingine mkubwa.
Kwasasa kasi imepungua na haijaeleweka kama Sangoma kakutana na ugumu au kuna tatizo gani.
Hii ndio bongo,na hili ndio soka la bongo na hao ndio makocha wetu wa kibongo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.