Saturday, October 12, 2013

Simba,Yanga zafukuzana,Ashanti yaonja ladha ya ushindi

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara imekamilisha raundi ya nane leo Oktoba 12 kwa mechi tatu zilizochezwa Dar es Salaam na Bukoba mkoani Kagera.

Katika uwanja wa Taifa bao pekee lililofungwa na Jonas Mkude limetosha kuwabeba Simba na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakifikisha pointi 18.

Mkude alifunga bao hilo baada ya kona iliyopigwa kwenye lango la Tanzania Prisons katika dakika ya 62 kuokolewa na kumkuta akiwa analitazama lango la maafande hao na kupiga mkwaju uliokwenda moja kwa moja wavuni.

Huko Kaitaba mkoani Kagera mabingwa watetezi Yanga Africa wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 yakiwekwa wavuni na Mrisho Khalfan Ngassa Anko na Hamis Kiiza Diego na kuwafanya Yanga kutimiza pointi 15.

Huko Azam Complex Chamazi Ashanti United Watoto wa Jiji wameonja ushindi wao wa kwanza baada ya kuifunga Coastal Union Mangushi kwa mabao 2-1.


Raundi ya tisa ya ligi hiyo inaanza kesho Jumapili Oktoba 13 mwaka huu kwa mechi kati ya Ruvu Shooting na Rhino Rangers (Mabatini, Mlandizi), Mgambo Shooting na Mbeya City (Mkwakwani, Tanga), Azam na JKT Ruvu (Azam Complex, Dar es Salaam) na Mtibwa Sugar na Oljoro JKT (Manungu, Turiani).


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.