CHELSEA wanajipanga kwenye dirisha dogo mwezi january kupeleka ofa Galatasaray ili kumnasa mshambuliaji Burak Yilmaz na wakipanga mpango huo kumuhusisha Demba Ba.
Ripoti kutoka Uturuki zinasema kuwa kocha Jose Mourinho anamtaka Yilmaz aliyehusishwa pia na Lazio,Arsenal na Liverpool wakati wa usajili uliopita lakini akaendelea kubakia Galatasary.
Mourinho muda mrefu amekuwa anamzimia mshambuliaji huyo na sasa yupo tayari kumtoa sadaka Ba ili kumpata.
Mourinho alielezwa kuwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 ana thamani ya paundi milioni 20 lakini dau hilo litapungua kwakuwa Ba atahusika.
Yilmaz ametupia wavuni mabao 32 katika mechi 39 alizoichezea Galatasaray msimu uliopita na Mourinho alimsifia mshambuliaji huyo wakati wa mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Real MaDRID akisema Drogba, Sneijder na Burak Yilmaz wanaweza kucheza kokote duniani.
Ba anaonekana hana nafasi ndani ya Chelsea na alihusishwa kutakiwa na Arsenal, West Ham, Newcastle na AS Roma kwenye usajili uliopita.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.