Thursday, October 3, 2013

VPL : Simba ushambuliaji kisu kikali,Ashanti jamvi la wageni,Coastal Union ukuta wa chuma


Msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara umeendelea kuwaweka kileleni wekundu wa Msimbazi Simba huku Ashanti United wakiendelea kuteseka mkiani.

Simba wanaendelea kuongoza ligi lakini pia wanaongoza kwa kufunga mabao mengi zaidi wakiwa na mabao 15 wakifuatiwa na Yanga wenye mabao 11,Azam FC nao wamo wakiwa na mabao 9.

Ashanti United ndio timu iliyobebeshwa mabao mengi zaidi wakiwa tayari wamekubali nyavu zao kutikiswa mara 15 wakifuatiwa na Mgambo JKT walioruhusu mabao 10.

Coastal Union ndio timu ambayo inaonekana ina ukuta mgumu zaidi kwa kukubali nyavu zao kutikiswa mara 2 wakifuatiwa na Kagera ambao nyavu zao zimetikiswa mara 3 tu.

TANZANIA FOOTBALL FEDERATION
VODACOM PREMIER LEAGUE (VPL) 2013/2014










NO TEAMS P W D L GF GA GD PTS
1 Simba SC 6 4 2 0 15 4 11 14
2 Kagera Sugar FC 6 3 2 1 7 3 4 11
3 Azam FC 6 2 4 0 9 6 3 10
4 Coastal Union FC 6 2 4 0 5 2 3 10
5 Young Africans SC 6 2 3 1 11 7 4 9
6 JKT Ruvu FC 6 3 0 3 6 4 2 9
7 Ruvu Shooting FC 6 3 0 3 6 4 2 9
8 Mbeya City SC 6 1 5 0 6 5 1 8
9 Rhino Rangers FC 7 1 4 2 7 8 -1 7
10 Mtibwa Sugar FC 6 1 4 1 5 6 -1 7
11 JKT Oljoro FC 6 1 2 3 3 6 -3 5
12 Mgambo Shooting FC 6 1 2 3 2 10 -8 5
13 Tanzania Prisons FC 6 0 4 2 3 9 -6 4
14 Ashanti United SC 7 0 2 5 4 15 -11 2

TOTAL 43 12 19 12 89 89 0 110

AS FOR: 29/09/2013









Avg of Goal per game 2.1






No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.