Mshambuliaji huyo anaendelea kuthibitisha kuwa yeye amezaliwa kutupia wavuni na akithibitisha kuwa yeye ni zaidi ya Cavani aliyesajiliwa kwa dau kubwa msimu huu.
Cavani amesajiliwa kwa paundi milioni 50 akitokea Napoli ya Italia akaweka rekodi kwa muda ya kusajiliwa kwa dau kubwa katika soka la Ufaransa rekodi ambayo ikavunjwa siku chache baadaye na Radamel Falcao aliyesajiliwa na Monaco kwa paundi milioni 54 akitokea Atletico Madrid.
Lakini Zlatan anaendelea kuthibitisha ubora wake.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.