Friday, October 11, 2013

Mercedes ya Hamilton yafanya kweli


Lewis Hamilton amemuongoza dereva mwenzake wa Mercedes Nico Rosberg katika majaribio ya kwanza ya Japanese Grand Prix.

Wawili hao wamemaliza mbele ya madereva wa Red Bulls Sebastian Vettel na Mark Webber.

Hamilton amemaliza mbele ya Rosberg kwa sekunde 0.330.

Madereva wa Ferrari Felipe Massa na Fernando Alonso wamemaliza kwenye nafasi ya tano na nafasi ya sita.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.