Friday, October 18, 2013

Murray apiga hesabu za kurudi kwenye Tennis

Mcheza Tennis Andy Murray amesema atacheza katika mashindano ya wazi ya Australia kama tu atakuwa fit kwa asilimia 100 baada ya kufanyiwa oparesheni ya mgongo.

Bingwa huyo wa Wimbledon alifanyiwa oparesheni hiyo mwezi uliopita.

Murray, 26, atakuwa nje kwa michezo ya mwisho ya msimu huko London lakini anataka kuwa tayari kwa Grand Slam ya kwanza 2014 huko Melbourne mwezi January.

Anasema kwasasa anafanya mazoezi kwenye swimming pool na kwa kutumia Baiskeli ambayo itamchukua wiki nne mpaka tano kabla ya kurejea kwenye viwanja vya Tennis na kuanza kuucheza tena.

Lakini hata hivyo Murray anasema hataki kurudi haraka kwenye Tennis anataka kuona akiwa amepona kwa asilimia 100 na hilo analitarajia kuwa mwanzoni mwa 2014.

Murray alijitokea kwenye michuano ya French Open mwezi May kwasababu ya maumivu lakini akarejea baada ya kupona na kushinda taji la Wimbledon na kumfanya kuwa Muingereza wa kwanza kuchukua taji hilo tokea mwaka 1936.

Lakini akashindwa kutetea taji lake la US Open akikwama kwenye hatua ya robo fainali baadaye akaisaidia Great Britain kuichapa Croatia kwenye Davis Cup kabla ya kufanyiwa upasuaji.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.