Mshambuliaji Samuel Eto'o amejiunga na kambi ya timu ya Taifa ya Cameroon huko nchini Ufaransa baada ya kuachana na maamuzi yake ya kustaafu kuichezea timu ya Taifa.
Nahodha huyo wa muda mrefu wa Cameroon na anayeongoza kwa kutupia wavuni atajiunga na wachezaji wenzake wengine kwenye kambi ya huko Lisses Ufaransa kwa mchezo wao wa hatua ya mtoano kuisaka tiketi ya kucheza kombe la dunia 2014 dhidi ya Tunisia.
Etoóanasema yeye ni mtu namba moja kurejea kwenye timu ya Taifa na kuhakikisha wanasaidiana kuivusha Cameroon kwenda fainali za kombe la dunia.
Mshambuliaji huyo alikuwa na kikao na katibu mkuu ofisi ya Rais Ferdinand Ngoh Ngoh,aliyekutana naye kwa niaba ya Rais Paul Biya.
Eto'o aliwambia wachezaji wenzake kuwa anajiweka pembeni kuitumikia timu ya Taifa kwasababu za kifamilia baada ya mchezo wa mwisho hatua ya makundi dhidi ya Libya uliochezwa huko Yaounde mwezi uliopita.
Mshambuliaji huyo amejiunga na Chelsea mwezi August akitokea Russian kwenye klabu ya Anzhi Makhachkala.
Ameshinda mataji matatu ya ligi ya mabingwa barani Ulaya,mara moja akiwa na Inter Milan na mara mbili akiwa na Barcelona.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.