Nyota wa ki Japan Keisuke Honda amesaini mkataba wa awali wa kujiunga na AC Milan wakati mkataba wake utakapokamalizika kwenye klabu ya CSKA Moscow ya Russia December 31.
Nyaraka inayohusiana na uhamisho wake wa bure imepelekwa kwa mamlaka za soka za Italia.
Makamu wa Rais wa AC Milan Adriano Galliani amesema kuwa tayari wamefanya mkataba wa awali na Honda na kweli nyaraka zimewasilishwa kwa mamlaka husika.
AC Milan wakati wa usajili wa majira ya joto walishindwa kumsajili mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 aliyeisaidia Japan kufika hatua ya 16 bora kwenye kombe la dunia 2010 baada ya CSKA kutaka dau la dola milioni 6.7 kwaajili ya uhamisho.
Timu nyingine zilizokuwa zinamtolea macho mshambuliaji huyo ni pamoja na Tottenham,Juventus, Monaco na Liverpool.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.