Tuesday, October 8, 2013
Poyet kocha mpya Sunderland
Timu ya Sunderland imemtaja aliyekuwa kocha wa Brighton Gus Poyet kuwa kocha wao mpya.
Sunderland The Black Cats,ambao wanaburuza mkia kwenye ligi kuu ya England EPL walimtimua kazi Paolo Di Canio baada ya kuiongoza timu hiyo kwa michezo 13 ya msimu uliopita na msimu huu.
Poyet, 45,amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake Stadium of Light.
Mwenyekiti wa Sunderland Ellis Short amesema wametazama kocha kwa mapana yake na kugundua miongoni mwa orodha yao Poyet ana rekodi nzuri,uzoefu,mwenye kuwajibika ,mapenzi ya kazi na hivyo wameona ndioye mtu sahihi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.