Thursday, October 17, 2013

Aboutrika ajiweka pembeni Misri

Mkongwe Mohamed Aboutrika anayechezea Al Ahly ya Misri anataraajia kutundika daruga mwaka huu.

Kwa mujibu wa Televisheni ya Al-Ahly ,Aboutrika mwenye miaka 34 atastaafu baada ya Al Ahly kukamilisha kibarua chake kwenye Champions League.

Wanacheza na Coton Sport ya Cameroon hapo Jumapili ikiwa ni mchezo wa marudiano nusu fainali baada ya kutroka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza.

Kama Al Ahly watafuzu watakutana na ama Esperance ya Tunisia au Orlando Pirates ya South Africa kwenye hatua ya fainali itakayopigwa November.

Mmoja wa wachezaji bora Africa ambaye hakuwahi kucheza Ulaya ,Aboutrika aliifungia Misri kwenye mchezo wa kuisaka tiketi ya fainali za kombe la dunia mchezo ulimalizika kwa Misri kula kibano cha mabao 6-1 Jumanne.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.