Chelsea imepataushindi wake wa kwanza kwenye Champions league msimu huu ikiibuka na ushindi wa mabao 0-4 dhidi ya wenyeji wao Steaua Bucharest Ramires akiingia wavuni mara mbili,Lampard mara moja na bao lingine Steaua wakijifunga wenyewe kufuatia mkwaju uliopigwa na Samuel Etoo.
Arsenal nao si haba wamepata ushindi wao wa pili kwenye chyampions league wakiichapa Napoli ya Rafa Benitez mabao 2-0 huku Mesut Ozil akianza kutumbukia wavuni.
Barcelona wakapata ushindi wa bao 1-0 kwa taabu huko Celtic Park mbele ya wenyeji wao Celtic ambao walilazimika kubaki kumi baada ya mchezaji wao mmoja kutolewa kwa kadi nyekundu.
Mario Balotelli akaibeba AC Milan isiaibike mbele ya Ajax baada ya kutupia wavuni penati iliyopatikana dakika za mwisho na mchezo kumalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.