Friday, October 25, 2013

Bafana bafana vs Hispania,kitu kinapigwa Jóburg


South Africa wanatarajia kucheza dhidi ya mabingwa wa Ulaya na dunia Hispania huko Johannesburg November 19 katika mchezo wa kirafiki.

Rais wa Chama cha soka cha Africa Kusini SAFA Dr Danny Jordaan,amesema ndoto zinaanza kuwa kweli kwa mashabiki kuanza kuwaona wachezaji kama Iniesta na Xavi wakiwa uwanjani.

Mchezo huo unataraji kupigwa kwenye dimba la Soccer City,uwanja ambao una historia ya kunyakuliwa kwa mara ya kwanza kwa kombe la dunia kwenye ardhi ya Africa.

Anasema huo ni mpango wake wa kuifanya Bafana Bafana kuigusa dunia kwa mara nyingine.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.