Friday, October 4, 2013

Afghanistan kucheza kombe la dunia kwa mara ya kwanza

Afghanistan watacheza fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2015 baada ya kuishinda Kenya kwa wickets saba kwenye mchezo wao wa mwisho wa kufuzu uliochezwa huko Sharjah.

Nchi hiyo ni moja ya nchi dhoofu duniani na iliyoathiriwa na migongano.

Wamefikia hatua hiyo wakimaliza nafasi ya pili nyuma ya Ireland na wametumbukia kwenye kundi moja na England,Australia na New Zealand.

Mchezo wao wa kwanza utakuwa dhidi ya Bangladesh huko Canberra February 18 2015 pia watacheza na Sri Lanka, Australia na New Zealand kabla ya kukutana na England huko Sydney March 13.

World Cup 2015 Pool A

England, Australia, Sri Lanka, Bangladesh, New Zealand, Afghanistan, qualifier

World Cup 2015 Pool B

South Africa, India, Pakistan, West Indies, Zimbabwe, Ireland, qualifier

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.