Tuesday, October 15, 2013

Simba yaipiga Yanga chenga


Mabingwa wa zamani wa Tanzania Wekundu wa Msimbazi Simba wameipiga chenga Yanga juu ya kambi yao kuelekea kwenye mchezo dhidi ya mahasimu wao hao utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Taifa.

Awali Wekundu hao walipiga hesabu za kwenda kupiga kambi visiwani Zanzibar lakini wakahairisha mpango wao wa kwenda huku baada ya kugundua kuwa Yanga wamekwenda kupiga kambi yao huko kisiwani Pemba Zanzibar.
Simba wao wakapiga hesabu na kusema kuwa kambi yao watakwenda kuweka huko Bagamoyo mkoani Pwani na wakatangaza kuwa jana ndio wangeingia kambini lakini kinyume chake Wekundu hao wameendelea kubakia Kigamboni Bamba beach.

Leo wameendelea na mazoezi yao huko huko Bamba beach ambako ndiko walipoweka kambi tokea kuanza kwa msimu.

Mechi za Simba na Yanga zinapokaribua huwa kuna mambo mengi na vitu vingi vinafanyika ikiwa ni kupotezana na kumficha hasimu wako sehemu ulipo na mara nyingi timu hizo zimekuwa zinahama kwenye kambi zao za awali.


Simba wanaongoza ligi wakiwa na pointi 18 huku Yanga wakiwa nafasi ya 4 nyuma ya Azam na Mbeya City wakiwa na pointi 15.

Kama Simba itafungwa na Yanga watafikisha pointi sawa sawa na kutofautiana kwa magoli ya kufunga na kufungwa na kama Yanga atafungwa atazidi kukimbiwa na Simba japo pia wakitoka sare mbio zao za kufukazana kwa tofauti ya pointi tatu zitaendelea.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.