Thursday, October 17, 2013

Yanga yajitabiria kumpiga Simba 3-0 Jumapili


KATIBU wa baraza la wazee klabu ya Yanga Ibrahim Omary Akilimali Abramovic ametamba kuwa lazima waifunge Simba Jumapili katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa Uwanja wa Taifa.

Akilimali amesema ahadi waliyoahidi ya kumfunga Simba mara tano mfululizo ndio ambayo wanaendelea kuitekeleza baada ya wao kuchapwa bao 5-0 na Wekundu hao.

Amesema wanaamini maumivu ya bao 5 kwa mara moja hayaumi sana kama maumivu ya kufungwa mechi 5 mfululizo kila wanapokutana.

Akilimali anasema katika mchezo huo wanaamini watapata ushindi wa mabao 3-0 mbele ya wekundu hao wa Msimbazi ambao wana machungu nao.

Tayari Yanga wameshashinda mchezo mmoja uliopita uliochezwa baada ya kutolewa kwa ahadi hiyo na baraza la wazee.

Yanga wamepiga kambi yao huko Pemba visiwani Zanzibar wakati Simba wao wamepiga kambi yao huko Bamba beach Kigamboni.

Simba wanaongoza ligi wakiwa na pointi 18 wakati Yanga wanakamata nafasi ya 4 nyuma ya Azam FC na Mbeya City wakiwa na pointi 15.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.