Thursday, October 24, 2013

Rooney arejesha furaha yake United huku akimchana Ferguson


Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney anasema kocha mpya wa kikosi hicho David Moyes amempa muelekeo mpya wa maisha.

Rooney alitaka kuondoka kwenye timu hiyo baada ya kukorofishana na kocha aliyestaafu Sir Alex Ferguson ambaye ameandika kwenye kitabu chake kuwa Rooney alipoteza uwezo wake wakati alipokuwa kwenye msimu wake wa mwisho kuifundisha United kwakuwa hakuwa fit vya kutosha.

Mshambuliaji huyo mwenyewe anasema anatazama mbele hayo mengine yalikwishapita.

Rooney, ambaye ansheherekea kuzaliwa kwake akitimiza miaka 28 aliisaidia United kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Real Sociedad baada ya beki Inigo Martinez kujifunga kwenye harakati za kuokoa mpira uliopigwa baada ya juhudi za Rooney.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tokea alipotibuana na Ferguson,Rooney,amesema hajaonana na Fergie tokea alipotangaza kustaafu kuifundisha timu hiyo.

Rooney anasema anafurahia maisha chini ya Moyes.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.