Thursday, October 3, 2013

MBELEKO : Hodgson asema Hart bado namba moja England


KOCHA wa England Roy Hodgson yupo nyuma ya kipa Joe Hart.

Kipa huyo wa Manchester City amekuwa akisakamwa baada ya kufanya madudu kwenye mchezo wa jana ligi ya mabingwa dhidi ya Bayern Munich mchezo uliomalizika kwa Bayern kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Lakini Hodgson anasema pamoja na kiwango alichoonesha jana kipa huyo bado ni namba moja kwake na hakuwahi kumuangusha.

Hart alionekana kushindwa kuzuia mipira iliyojaa wavuni ya Franck Ribery na Arjen Robben kiasi cha kuzua maswali juu ya kiwango chake.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.