Friday, October 11, 2013

Dereva wa Formula1 akutwa amekufa hotelini

Dereva wa akiba wa mbio za magari za Formula1 Langalanga Maria De Villota amekutwa amekufa kwenye chumba cha hoteli huko Seville,nchini Hispania.

Msemaji wa jeshi la Polisi amesema wanafikiria kuwa kifo hicho ni cha kawaida lakini bado hawajathibitisha.

De Villota, 33,itakumbukwa alipoteza jicho lake la kuliwa kwenye ajali mwezsi July wakati akifanya majaribio na timu ya Marussia.
Aliumia kichwani na usoni baada ya kugongana na lori lakini akaruhusiwa kurejea tena kuendesha magari.

De Villota,amekuwa akishirikishi kwenye mbio za magari kwa miaka 12 hapo kabla ameendesha katika mbio za Formula3 kabla ya ndoto yake ya kushindan kwenye Formula1 kutimia miaka miwili iliyopita.
De Villota, binti wa dereva wa zamani wa Formula1 Emilio,ameripotiwa kuwa alikuwa huko Seville kuzindua autobiography yake.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.