Wambach amefunga ndoa hiyo na Sarah Jumamosi iliyopita huko Hawaii.
Mwezi June, Wambach, 33, aliweka rekodi ya kuwa mfumania nyavu wa wakati wote aliyetupia mabao mengi zaidi kwenye timu ya Taifa ya wanawake na wanaume akitupia jumla ya mabao 160 akivunja rekodi ya awali ya mabao 158 iliyowekwa na Mia Hamm.
Wambach,mwanasoka bora wa FIFA wa dunia kwa wanawake 2012 aliisaidia timu ya Taifa ya Marekani kushinda medali ya dhahabu kwenye Olympic iliyochezwa London mwaka uliopita.
Wawili hao Wambach na Sarah wamecheza kwenye timu moja ya Western New York Flash msimu uliopita wakiiwakilisha kwenye ligi ya soka ya wanawake ya taifa huko Marekani.
Kupitia mtandao wake wa twitter Abby Wambach amewashukuru wote kwa kumuunga mkono akionesha furaha yake.
Hiki ndicho alichoandika Wambach
Abby Wambach
Sarah and I wanted to thank everyone for all the love and support. We couldn't be happier. What an amazing week it's been. #honeymoon
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.