Mshambuliaji wa zamani wa MANCHESTER CITY Mtaliano Mario Balotelli anaweza akafanya uhamisho wa kushtua kuhamia Chelsea kwa mujibu wa wakala wake.
Balotelli,ambaye kwasasa anacheza AC Milan alikuwa pamoja na Jose Mourinho kwenye timu ya Inter Milan mwaka 2009.
Wakala wa Balotelli Mino Raiola amesema upo uwezekano mkubwa wa mshambuliaji huyo kuungana tena na Mourinho kwakuwa wawili hao hawakuachana kwa matatizo.
Anasema hakukuwa na matukio mazuri baina ya wawili hao lakini pia waliachana kwa makubaliano mazuri,kuna mawasiliano wanafanya na kuna heshima kati yao.
Wakala huyo anasema anafahamu makamu wa Rais wa AC Milan Adriano Galliani hatakubali lakini Balotelli ni mchezaji mkubwa.
Balotelli amefunga mabao 6 kwa klabu na timu yake ya Taifa kwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.