Friday, October 25, 2013

UBAGUZI : Toure ataka weusi wasusie kombe la dunia,Mourinho,Wenger nao watoa kauli


KIUNGO wa Manchester City Yaya Toure amesema Fifa na Uefa wafanye kazi yao baada ya mashabiki wa CSKA Moscow kufanya ubaguzi wa rangi kwake huku akitamani fainali za dunia 2018 zisusiwe kuonesha kukerwa na kitendo hicho.

Baada ya mchezo dhidi ya CSKA Moscow ,Toure alisema wachezaji wenye asili ya Africa wasikubali kucheza kwenye fainali hizo za 2018 zitakazofanyika Russia kama hakuna cha kufanya kukomesha vitendo vya kibaguzi.
Lakini makocha wa vilabu kadhaa vya Engtland wamesema kususia fainali hizo sio sawa pia kinaonesha kutopevuka.

Boss wa Chelsea Jose Mourinho amesema kususia fainali hizo za dunia 2018 sio njia ya kuondoa ubaguzi katika soka na akiwataka wachezaji kutowahukumu mabilioni kwasababu ya tabia isiyoyo na heshima ya maelfu.
Mourinho akahoji kipi muhimu mabilioni ya watu wanaopenda mpira au maelfu wachache wanaaokwenda viwanjani na taabia za hovyo zinawahusisha wachezaji weusi.

Akasema kama angekuwa mchezaji mweusi angetoa kipaumbele kwa mabilioni na angesema wacha tupigane na maelfu lakini tuwape mabilioni wanachohitaji.

Mourinho anasema kama hakuna wachezaji weusi pia hakuna ladha ya soka.

Manuel Pellegrini kocha wa Manchester City yeye akataka Uefa kushughulikia suala hilo na akisema anaamini halitatokea kwa mara nyingine.
Boss wa Arsenal, Arsene Wenger amesema Uefa wanatakiwa kukamilisha uchunguzi wao kabla ya kufikia mazungumzo ya kususia fainali za dunia 2018.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.