Monday, October 7, 2013

Kocha Herve Renard aitema Zambia Chipolopolo

Kocha Herve Renard ametema kibarua cha kuifundisha timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo na kujiunga na klabu ya FC Sochaux ya Ufaransa.

  Renard alkirejea kuifundisha Zambia kwa mara ya pili October 2011 na kuiongoza Chipolopolo kuchukua taji la Africa miezi minne baadaye japo ikashindwa kutetea taji lake na imeshindwa kufuzu hatua ya mtoano ya kuisaka tiketi ya fainali za kombe la dunia.

Zambia imemteua Patrice Beaumelle kama mbadala wa muda wa Renard.

Beaumelle,alikuwa kocha msaidizi na ataanza kibarua kwa kukiongoza kikosi hicho katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Brazil huko Beijing 15 October.

Taarifa ya chama cha soka cha Zambia FAZ imesema imekubaliana na kocha huyo kwakuwa amepata ofa kubwa kutoka kwa FC Sochaux na kwao ni fahari kwa kocha anayefundisha Africa kupata kazi ya kufundisha klabu kubwa kama hiyo.

Renard, 45, alipewa kibarua cha kuinoa Zambia kwa mara ya kwanza mwaka 2008 na kuipeleka mpaka robo fainali ya fainali za Africa 2010 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufika hatua hiyo baada ya miaka 14.

Baada ya hapo akaondoka na kwenda Angola kabla ya kujiunga na  USM Alger na baadaye akarejea tena kuifundisha Zambia akiiongoza kuchukua taji la Africa 2012.

Akiwa na Sochaux, anaungana na mshambuliaji wa Zambia Emmanuel Mayuka, anayecheza kwenye klabu hiyo kwa mkopo akitokea Southampton ya England.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.