Shirikisho la soka duniani FIFA limewajumuisha wachezaji 6 wa klabu ya Bayern Munich kwenye orodha ya wachezaji wengine 23 watakaowania tuzo la mchezaji bora duniani mwaka huu Ballon d'Or .
Jose Mourinho amejumuishwa kwenye orodha ya kocha bora licha ya kukosa kuiwezesha klabu ya Real Madrid kushinda taji lolote kubwa msimu uliopita, matokeo ambayo aliyataja kuwa mabovu.
Mchezaji wa pekee kutoka Uingereza ambaye ameteuliwa ni mchezaji wa kimataifa wa Wales, Gareth Bale.
Mshindi wa tuzo ya kocha bora Afrika Stephen Keshi wa Nigeria hakufanikiwa kuwa kwenye orodha hiyo huku mwafrika pekee kuteuliwa kuwania taji hilo akiwa Yaya Toure mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester City raia wa Ivory Coast.
Kwenye orodha hiyo hamna wawakilishi kutoka Asia ama CONCACAF
Wachezaji wa kimataifa kutoka Ujerumani Manuel Neuer, Bastian Schweinsteiger , Thomas Mueller na Phillip Lahm pamoja na mfaransa Franck Ribery na mchezaji wa Uholanzi Arjen Robben ndio wachezaji wa Bayern walioteuliwa.
Wengine waliojumuishwa kwenye orodha hiyo ni wachezaji maarufu kama Lionel Messi, Andres Ineasta na Cristiano Ronaldo.
Aliyekuwa kocha wa Bayern Jupp Heynckes ambaye nafasi yake imechukuliwa na Pep Guardiola ameteuliwa kwenye orodha ya kocha bora baada ya kuiongoza klabu yake kushinda ligi ya ujerumani ya Bundesliga, kombe la ujerumani na ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Fifa world men's player of the year shortlist:
Gareth Bale (Real Madrid/Wales), Edinson Cavani (Paris
St-Germain/Uruguay), Radamel Falcao (Monaco/Colombia), Eden Hazard
(Chelsea/Belgium), Zlatan Ibrahimovic (Paris St-Germain/Sweden), Andres
Iniesta (Barcelona/Spain), Philipp Lahm (Bayern Munich/Germany), Robert
Lewandowski (Borussia Dortmund/Poland), Lionel Messi
(Barcelona/Argentina), Thomas Muller (Bayern Munich/Germany), Manuel
Neuer (Bayern Munich/Germany), Neymar (Barcelona/Brazil), Mesut Ozil
(Arsenal/Germany), Andrea Pirlo (Juventus/Italy), Franck Ribery (Bayern
Munich/France), Arjen Robben (Bayern Munich/Netherlands), Cristiano
Ronaldo (Real Madrid/Portugal), Bastian Schweinsteiger (Bayern
Munich/Germany), Luis Suarez (Liverpool/Uruguay), Thiago Silva (Paris
St-Germain/Brazil), Yaya Toure (Manchester City/Ivory Coast), Robin Van
Persie (Manchester United/Netherlands), Xavi (Barcelona/Spain).
Fifa coach of the year shortlist:
Carlo Ancelotti (Real Madrid), Rafael Benítez (Napoli), Antonio
Conte (Juventus), Vicente Del Bosque (Spain), Sir Alex Ferguson
(Manchester United's former manager), Jupp Heynckes (Bayern Munich's
former coach), Jurgen Klopp (Borussia Dortmund), Jose Mourinho
(Chelsea), Luiz Felipe Scolari (Brazil), Arsene Wenger (Arsenal).
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.