Hoffenheim wanagomea goli la Bayer Leverkusen baada ya mpira wa kichwa uliopigwa na Stefan Kiessling kupitia pembeni ya wavu na kutinga wavuni kwa kutumia tundu lililopo kwenye nyavu.
Mwamuzi Felix Brych hakuweza kutambua kama mpira huo uliopigwa na Kiessling ulipita pembeni katika dakika ya 70 ya mchezo na Leverkusen wakashinda mabao 2-1 kwenye ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga iliyochezwa jana usiku.
Mkurugenzi mtendaji wa Hoffenheim Alexander Rosen yeye ameiita kama ni skendo akisema halikuwa goli halali na wanataka marudio ya kwenye Tv ya goli hilo.
Brych,ambaye ni mwamuzi mwenye beji ya Fifa yeye anasema alikuwa na mashaka lakini mapokeo ya wachezaji akaona yapo tofauti hakuna hata mmoja aliyekuwa anatilia shaka goli hilo na hakuna aliyekuwa kinyume na maamuzi yake ya kuhesabu goli.
Tukio kama hilo limewahi kutokea April 1994, Bayern Munich ilipoifunga Nuremburg 2-1 baada ya beki Thomas Helmer alipozawadiwa goli wakati mpira haukuingia wavuni.
Nuremburg wakawasilisha malalamiko kwa Chama cha soka cha Ujerumani na mchezo ukarudiwa na Bayern wakashinda 5-0.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.