Wednesday, October 30, 2013

Real Madrid yamtoa sadaka Benzema impate Suarez

REAL MADRID wanajipanga kwa usajili wa dirisha dogo mwezi January kutumbukia kumnasa Luis Suarez wa Liverpool kwa dau la paundi milioni 20 pamoja na mshambuliaji Karim Benzema.

Suarez bado inaelezwa anataka kuondoka Anfield,licha ya mwanzo mzuri wa msimu kwa Liverpool.

Arsenal nao wanajipanga kwa dau lingine baada ya kutolewa nje kwenye usajili uliopita wa majira ya joto.

Lakini Suarez inaonekana anapenda zaidi kwenda Real Madrid inayofundishwa na Carlo Ancelotti na wakali hao wa Hispania wana matumaini ya kuwashawishi Liverpool kwa kuwapa fedha na mchezaji mwenye jina kubwa Benzema.

Madrid wanaona thamani ya Benzema ni paundi milioni 20 inayofanya mpango huo kuwa na jumla ya paundi milioni 40.
 

Benzema tayari anaonekana kupoteza thamani yake ndani ya Real Madrid na tayari ameambiwa anaweza kuondoka na kusaka timu nyingine.

Madrid wametumia kiasi cha paundi milioni 150 kwenye usajili wake ikiwemo paundi milioni 86 walizozitoa kumnunua Gareth Bale aliyeweka rekodi ya dunia kwakuwa mchezaji ghali zaidi.


Fabio Coentrao, Sami Khedira na Angel Di Maria ni miongoni mwa wale wanaotajwa kuwa sehemu ya kuuwezesha mpango wa kumnasa Suarez.
 
 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.