Friday, October 4, 2013

Hamilton atesa kwenye Formula1 langalanga

Dereva wa Mercedes Lewis Hamilton amemshinda bingwa wa dunia dereva wa Red Bull Sebastian Vettel na kujiweka vizuri katika siku ya pili ya majaribio ya Korean Grand Prix.

Hamilton alimaliza akimzidi Vettel kwa sekunde 0.108 huku Nico Rosberg akimaliza nafasi ya tatu na dereva wa pili wa Red Bull Mark Webber akamaliza nafasi ya nne.
Dereva wa Ferrari Felipe Massa amemaliza nafasi ya 5 akifuatiwa na dereva Fernando Alonso na Romain Grosjean.

Dereva wa Lotus Kimi Raikkonen akamaliza nafasi ya nane mbele ya dereva wa McLaren Jenson Button.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.