Tuesday, October 1, 2013

Kocha wa Ashanti aachia ngazi


Kocha mkuu wa Watoto wa JIJI Ashanti United Hassan Banyai ametangaza kuachia ngazi kuifundisha timu hiyo

Banyai amesema ameamua kwa mapenzi yake binafsi kujiweka pembeni kwa manufaa ya Ashanti United ambayo inacheza mechi za ligi bila ya kuwa na kocha baada ya yeye binafsi kukabiliwa na matatizo ya kifamilia.


Amesema mama yake mzazi ni mgonjwa kitu kinachomfanya ashindwe kuwajibika inavyopasa kwenye timu hiyo na ndio maana ameamua kutangaza kujiweka pembeni ili timu hiyo itafute kocha mwingine wa kuisukuma mbele.

Banyai amesema katika wakati huu ambao anamuuguza mama yake atakuwa anafundisha katika timu yake ya watoto ya kwenye Academy yake iliyopo Kigamboni.

Hata hivyo Banyai amekanusha kuikimbia Ashanti kwakuwa inafanya vibaya akisema aeleweke kuwa ni kwasababu ya matatizo ya kifamilia.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.