Thursday, October 31, 2013

Simba mikononi mwa Kagera Sugar,..kurushwa live Channel ten,TBC2

Wekundu wa Msimbazi Simba leo wanashuka dimbani kusaka pointi tatu muhimu za kutuliza mzuka huko Msimbazi baada ya kupata kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo uliopita dhidi ya Azam FC.

Simba wanashuka kuwakabili Kagera Sugar wana Nkurukumbi kwenye uwanja wa Taifa katika mchezo muhimu wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Wekundu hao wanashuka dimbani huku wakiwa wameshushwa kwenye msimamo wa ligi mpaka nafasi ya nne kufuatia Azam,Mbeya City na Yanga kushinda katika michezo yao iliyopita.

Azam wanaongoza wakiwa na pointi 23 sawa na Mbeya City,huku Yanga akikaa nafasi ya tatu akiwa na pointi 22 na Simba wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi 20.

Mchezo huo utarushwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC2 na Channel ten.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.