Boss wa Manchester City Manuel Pellegrini amehoji maamuzi ya Uefa kuruhusu mchezo wao wa leo wa Champions League kundi D dhidi ya CSKA Moscow kuchezwa.
Hali ya uwanja wa Khimki Arena sehemu ya kuchezea ni ya hovyo baada ya kunyesha kwa mvua kubwa.
Pellegrini kocha wa zamani wa Malaga anasema haamini kama mchezo wa mashindano muhimu unaweza kuchezwa kwenye uwanja mbovu.
Anasema alidhani watu wa Uefa waliotazama uwanja huo wasingeruhusu mchezo huo kuchezwa hapo.
Mapema mwezi huu Uefa iliiamuru timu hiyo ya mji wa Moscow kucheza mchezo wake wa nyumbani dhidi ya Viktoria Plzen huko St Petersburg kwasababu ya ubovu wa uwanja.
Meneja wa CSKA Leonid Slutsky ambaye kikosi chake kimepoteza michezo mitano katika michezo saba iliyopita amekiri kuwa hali ya uwanja huo ni mbovu.
Slutsky,anasema hali ya uwanja ilivyo ni sawa na matokeo ya michezo yao iliyopita.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.