Monday, October 21, 2013

Bao lililosababishwa na Etoó laendelea kuwatesa Cardiff

Cardiff City wanataka kusaka maelezo zaidi kutoka kwa mtaalamu wa waamuzi Mike Riley, kujua kwanini mwamuzi Anthony Taylor, aliruhusu goli la kusawazisha la Chelsea Jumamosi kwenye mchezo wa ligi kuu ya Engrand.

Cardiff walikuwa wanaongoza wakati golikipa wa timu hiyo David Marshall,alipodunda mpira ili apige kwa wachezaji wenzake kabla ya Samuel Eto'o kuuwahi na kuuiba akampasia Eden Hazard akatupia wavuni kuisawazishia Chelsea.
Sheria inasema mpira unakuwa kwenye himaya ya kipa mpaka pale unapogusa ardhi na kocha wa timu hiyo Malky Mackay anasema waamuzi walikuwa kimya na walikubali bao bila utata.
Magolikipa wa timu zote mbili Marshall kwa Cardiff na Petr Cech kwa Chelsea hawakuweza kuelewa sheria ya mchezo kwa tukio kama lile inasemaje lakini Cech akasema kitendo cha Eto'o kilikuwa cha kutumia akili sana na kisicho cha kawaida.
Marshall kipa wa Cardiff anasema kitendo hicho kinamfanya aache mtindo wa kudunda mpira karibu na mchezaji wa timu pinzani,anasema alimuona Eto'o,na alijua yuko pale lakini tabia ya mazoea ikamfanya aendelee na yake na alijiona mkosefu kiasi cha kuomba radhi kwa wachezaji wenzake wakati wa mapumziko.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.