Kiungo mshambuliaji anayewaniwa na ARSENAL na Manchester United Wesley Sneijder ameambiwa ajiunge na Chelsea na kocha wa sasa wa timu ya Taifa ya Uholanzi Louis van Gaal.
Kiungo huyo mchezeshaji kwasasa anatoa huduma yake kwa Galatasaray,na aliisaidia timu yake ya Taifa ya Uholanzi iliposhinda dhidi ya Uturuki kwenye mchezo wa kuisaka tiketi ya fainali za kombe la dunia 2014.
Sneijder,anayewaniwa kwa muda mrefu na Arsenal na Man United,ametakiwa kuondoka Garatasary na badala yake ajiunge na kocha wake wa zamani wa Inter Milan Jose Mourinho ambaye sasa yupo na kikosi cha Chelsea.
Van Gaal amesema anafahamu kuwa Chelsea na Jose Mourinho wanahitaji huduma ya Sneijder,kwa mawazo yake kama kuna uwezekano kiungo huyo aondoke Galatasaray na kujiunga na Chelsea.
Anasema kiungo huyo akicheza chini ya Mourinho kwa mara nyingine ataboresha kiwango chake na atamsaidia kukiboresha kiwango chake hata kwa timu ya Taifa.
Kiungo huyo mwenye miaka 29 akiwa na Mourinho huko Inter Milan walifanikiwa kushinda mataji kadhaa ikiwemo lile la Champions League walipoichapa Bayern Munich 2010.
Sneijder alijiunga na Galatasaray mwezi January kwa ada ya Euro milioni 7.5 baada ya miaka minne ya kucheza Italia.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.