Thursday, October 10, 2013

Madrid wampigia hesabu Ramires

Real Madrid wanajipanga kupeleka dau la paundi milioni 15 ili kumnasa kiungo wa Chelsea Ramires kwenye usajili wa dirisha dogo mwezi January.

Bosi wa Real Madrid Carlo Ancelotti kwasasa anapanga mipango ya mwaka mpya na tayari amewaambia ma scout wanaosaka vipaji kumtazama kiungo huyo raia wa Brazil.

Ancelotti kwasasa anamsaka kiungo wa kucheza karibu na eneo la adui box-to-box midfielder,akiwa na mashaka kwa kiungo wake Xabi Alonso.
Madrid tayari wamehusishwa na viungo kadhaa wakiwemo Paulinho wa Spurs,lakini inaaminika pia jicho lake lipo kwa Ramires zaidi.

Ramires alitua Chelsea wakati Ancelotti akiwa kocha wa kikosi hicho na inaonekana kuwa kiungo huyo mwenye miaka 26 anapenda kuungana tena na bosi wake wa zamani.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.