Thursday, October 3, 2013

Ethiopia v Nigeria,Fifa yataja waamuzi,Musonye naye ndani


Shirikisho la soka duniani Fifa imewatangaza waamuzi wa mchezo wa mtoano kombe la dunia kati ya Ethiopia na Nigeria utakaopigwa October 13 kwenye uwanja wa Taifa huko Addis Ababa.

Fifa pia wamethibitisha kuwa mchezo huo utachezwa saa 10 jioni tofauti na taarifa za awali zzilizosema kuwa mchezo huo utachezwa saa 8 mchana.

Alioum Neant atakuwa muamuzi wa kati akisaidiwa na Evarist Menkouande na Yanoussa Moussa huku muamuzi wa mezani akiwa Kalla Henry Duvalier.

Fifa pia imemtaja kamishna wa mchezo huo kuwa anatoka Zimbabwe Wilfred Mukuna afisa wa usalama kutoka Kenya Nicholas Musonye na muangalizi wa Fifa kutoka Switzerland Walter Gagg.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.