KIUNGO wa Manchester City Yaya Toure amekasirika na ameitaka Uefa kuchukua hatua juu ya ubaguzi aliofanyiwa na mashabiki wa nyumbani wakati walipoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wao CSKA Moscow kwenye Champions league.
Yaya anasema alimwambia mwamuzi Ovidiu Hategan kuhusu kelele za kibaguzi wakati City ikitoka nyuma na kushinda kwa mabao ya Sergio Aguero katika mchezo huo wa kundi D.
Anasema si tu amekatishwa tamaa pia amekasirika.
Anasema amekasirika kwa kitendo cha mashabiki hao walichokifanya huku akiwa amevaa kitambaa cha unahodha tena kikiwa kinapiga vita ubaguzi wa rangi.
Alipoulizwa ni hatua gani yapasa kuchukuliwa akasema yawezekana labda uwanja ufungiwe kwa miaka kadhaa au miezi kadhaa na hilo ni jambo kubwa na lazima kuwa na maamuzi thabiri vinginevyo wataendelea na mchezo huo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.