NYOTA wa Ivory Coast Didier Drogba anakwenda nyumbani na sifa kubwa ya kiatu cha dhahabu baada ya kupata tuzo hiyo huko Monaco baada ya jina lake kuwa juu ya majina mengine makubwa kama Cristiano Ronaldo, Andres Iniesta na mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea Frank Lampard katika tuzo iliyopigwa na wachambuzi wa soka.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 35 anayecheza Galatasaray amepewa tuzo hiyo inayotolewa kila mwaka kwa wachezaji walio na umri wa kuanzia miaka 28 ambao bado wanafanya vizuri.
Drogba pia anakuwa mchezaji wa pili aliyecheza ligi ya England kupata tuzo hiyo ya kiatu cha dhahabu baada ya Ryan Giggs wa Manchester United.
Drogba ataweka alama ya mguu wake huko Monaco ambako pia tayari kuna majina makubwa yameshawahi kufanya hivyo ikiwemo Ronaldo, Del Piero, Nedved na Roberto Baggio.
Mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coasta anakuwa mchezaji wa kwanza kutokea Africa kupata tuzo hiyo ambayo mwaka uliopita ilichukuliwa na mshambuliaji wa Paris Saint German Zlatan Ibrahimovic.
Waliokuwa wakiwania tuzo hiyo kwa mwaka 2013 ni Cristiano Ronaldo, Andres Iniesta, Frank Lampard, David Trezeguet, Andrea Pirlo, Samuel Eto’o, Iker Casillas, David Beckham, Miroslav Klose.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.