Tuesday, October 15, 2013

Jembe Messi larejea Barcelona

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amerejea kwenye mazoezi baada ya kukaa nje kwakuwa na maumivu.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 26 aliumia kwenye mchezo ambao Barcelona ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Almeria September 28.

Messi mpaka sasa kashatumbukia wavuni mara 8 katika mechi 6 za ligi kuu alizocheza msimu huu na amefunga hat-trick dhidi ya Ajax kwenye Champions League.

Alikosa Champions League Barcelona ilipocheza na Celtic na alikosa mchezo wa La Liga wakishinda dhidi ya Valladolid,pia yupo nje ya kikosi cha Argentina.

Argentina tayari wamefuzu kucheza fainali za dunia 2014 nchini Brazil.

Mwanasoka bora wa mwaka wa dunia Messi ameanza mazoezi yake jana akiwa na kikosi cha Barcelona chini ya kocha Gerardo Martino.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.