Thursday, October 31, 2013
Mabomu ya machozi yarindima uwanja wa Taifa,Simba ikishikwa na Kagera,mashabiki wavunja viti
Kuvunjwa kwa viti na kupigwa kwa mabomu ya machozi ni moja ya matukio yaliyotokea kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya wekundu wa Msimbazi Simba dhidi ya Kagera Sugar wana Nkurukumbi uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa Dar Es Salaam uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Polisi walilazimika kupiga mabomu ya machozi baada ya mashabiki wa Simba kuanzisha vurugu na kuvunja viti vya uwanja huo hali iliyolazimu kuanza kupigwa kwa mabomu ya machozi ili kuwatawanya mashabiki hao.
Mpaka viti vinavunjwa na mabomu yanaanza kupigwa Simba na Kagera walikuwa wamefungana bao 1-1.
Bao la Simba limefungwa na Amis Tambwe wakati lile la Kagera lilipachikwa wavuni na Salum Kanoni Kupela kwa mkwaju wa penati baada ya kuangushwa ndani ya kisanduku kwa mshambuliaji Adam Kingwande.
Simba sasa wanafikisha pointi 21 wakiendelea kukaa nyuma ya Azam FC,Mbeya City wenye pointi 23 na Yanga wenye pointi 22 huku Simba akicheza mchezo mmoja zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.