Arsenal wameambiwa wanaweza kumnasa mshamabuliaji wa Real Madrid Karim Benzema wakati wa uhamisho wa dirisha dogo mwezi January kwakuwa wakali hao wa Hispania wanapanga kutumbukia kumfukuzia Luis Suarez.
Klabu hiyo ya Kaskazini mwa London walijaribu kumfukuzia mshambuliaji huyo wakati wa usajili wa majira ya joto lakini ikashindikana.
Carlo Ancelotti amepoteza matumaini kwa mshambuliaji huyo ambaye ametupia wavuni mabao mawili katika mechi nane.
Rais wa Real Madrid Florentino Perez anafahamu kuwa licha ya kufanya usajili wa rekodi kumnasa Gareth Bale,bado safu ya ushambuliaji inahitaji kuongezwa nguvu na anapanga kumuuza Benzema nyota wa zamani wa Lyon aliyewagharimu paundi milioni 30 mwaka 2009.
Real Madrid wanataka kurudi kumshawishi Suarez atue kwenye klabu hiyo japo pia wamemtaja mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero kama chaguo lingine ambalo wanalitazama.
Ripoti wiki hii zinasema kuwa Suarez amewaambia marafiki zake kuwa bado anataka kuondoka Anfield.
Maboss wa Liverpool walikataa ofa ya Arsenal waliotaka kumnasa Suarez wakati wa usajili wa majira ya joto wakisema hauzwi lakini MADRID wanaamini kuwa January wanaweza kumchukua kwa dau sahihi.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.