Radamel Falcao ameshindwa kukanusha taarifa za kutakiwa kwake na Real Madrid kwa dau nono wakati wa usajili ujao wa majira ya joto.
Mshambuliaji huyo raia wa Colombia ameahamia Monaco msimu huu lakini mapema wiki hii Rais wa Real Madrid Florentino Perez amesema watapeleka ofa mwishoni mwa msimu kujaribu kumnasa mshambuliaji huyo.
Perez pia amesema tayari amemwambia Falcao,ambaye amefunga mabao 7 katika mechi 9 za ligi kuu ya Ufaransa Ligue 1 kuhusu mipangto hiyo.
Falcao yeye anasisitiza anafuraha ndani ya Monaco,ambao waliilipa Atletico Madrid paundi milioni 50 kwaajili ya kupata huduma yake japo hajapinga kurejea tena kusukuma gozi Hispania huku akimshukuru Perez kwa maneno yakeambayo yamemfanya ajisikie vizuri lakini anasema anaheshimu mkataba wake na Monaco .
Kutakiwa kwa Falcao kunaweza kuwafanya Real Madrid kuachana na mpango wao wa kumchukua mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.