Friday, October 4, 2013
Kolo Toure arudi mzigoni
Kolo Toure amejumuishwa tena kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tembo wa Ivory Coast kitakachocheza mchezo wa hatua ya mtoano kuisaka tiketi ya fainali za kombe la dunia dhidi ya Simba wa Teranga Senegal.
Beki huyo mwenye miaka 32 anayechezea Liverpool ya England hakuitwa kwenye timu ya Taifa tokea mwezi March,na sasa amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 24 kitakachoshuka dimbani kwenye mchezo huo wa October 12 utakaopigwa Abidjan.
Kiungo wa pembeni wa St Etienne Max Gradel ni miongoni mwa waliojumuishwa kikosini huku pia kocha Sabri Lamouchi akiwajumuisha wakongwe Didier Drogba na Didier Zokora.
Ivory Coast squad:
Goalkeepers: Boubacar Barry (Lokeren), Abdoul Karim Cisse (Africa Sports), Sylvain Gbohouo (Sewe Sport)
Defenders: Jean Akpa Akpro, Serge Aurier (both Toulouse), Arthur Boka (VfB Stuttgart), Benjamin Brou Angoua (Valenciennes), Soulemanye Bamba (Trabzonspor), Viera Diarrassouba (Caykur Rizespor), Kolo Toure (Liverpool), Didier Zokora (Trabzonspor)
Midfielders: Serey Die (Basel), Jean-Jacques Gosso Gosso (Genclerbirligi), Max Gradel (St Etienne), Didier Ya Konan (Hanover 96), Romaric (Bastia), Cheick Tiote (Newcastle United), Yaya Toure (Manchester City)
Forwards: Wilfried Bony (Swansea City), Didier Drogba (Galatasaray), Gervinho (AS Roma), Salomon Kalou (Lille), Giovanni Sio (VfL Wolfsburg), Lacina Traore (Anzhi Makhachkala).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.