Friday, October 11, 2013

Kocha aangusha machozi baada ya kutimuliwa kazi


Waziri wa kazi wa Msumbiji Helena Taipo amemtimua kazi kocha raia wa Ureno baada ya kuitukana nchi hiyo ambayo ni koloni la zamani la Ureno.

Kocha huyo Diamantino Miranda, aliyekuwa akiifundisha klpabu ya Costa do Sol yenye maskani yake Maputo anatakiwa kuondoka kesho Jumamosi.
Mwezi uliopita alirekodiwa akisema kuwa Msumbiji nhji kundi la wezi wakati alipokuwa anapinga maamuzi ya refa.

Miranda ameomba radhi mbele ya waandishi wa habari huku akilia akitangaza kuondoka nchini humo.

Amesema hakufahamu kama maneno yake yalikuwa yanarekodiwa huku akisema amewakamata watu wa msumbiji katika moyo wake.

Anaongeza kuwa ukweli utajulikana na ipo siku atarudi Msumbiji.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.