Sunday, October 27, 2013

Man U yasita kutoa dau kubwa kwa Rooney,Spurs,Arsenal watiana pembe,Mourinho kicheko

Sababu ya Manchester United kutokubaliana mkataba mpya na Wayne Rooney ni kutotaka kujitia kitanzi cha kumpa dau nono la paundi milioni 70 ili mshambuliaji huyo abaki Old Trafford.

Rooney anataka mshahara wake uongezeke kutoka ule wa sasa anaolipwa paundi 250,000 kwa wiki na anataka mkataba wa miaka mitano ili abakie.
Licha ya kiwango cha Rooney kuwa juu kwasasa baada ya kuporomoka baada ya mtifuano wake na kocha aliyeondoka Sir Alex Ferguson,bado klabu hiyo haitaki kutumia kitita kikubwa kwa mchezaji ambaye tayari ana miaka 28.

Rooney alikataliwa kuondoka kwenye usajili uliopita huku tayari Chelsea na Paris St Germain zikiwa zimemtolea macho na kocha wa sasa David Moyes akasema mshambuliaji huyo hauzwi kwa Chelsea ambao walipeleka ofa tatu na sasa inaonekana kwenye usajili wa dirisha dogo mwezi January inaweza kuibuka tena.
Upande mwingine Arsenal wako tayari kupigana na Tottenham kwa mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke wakati wa usajili wa dirisha dogo mwezi January.

The Gunners wanaendelea na kampeni zake za kulisaka taji msimu huu japo inaonekana inahitaji mshambuliaji mwenye kiwango cha dunia ili kutimiza lengo lake.
 
Naye mshambuliaji wa Real Madrid aliyepoteza mvuto Karim Benzema anaweza kutua kwenye ligi ya England kwa dau la paundi milioni 42.

Madrid wanataka kurudisha sehemu ya fedha walizotoa kumnunua Gareth Bale kwa kumuuza Benzema na inaelezwa kuwa klabu za Tottenham, Arsenal na Chelsea zimepewa taarifa za uwepo wa mshambuliaji huyo.
Hata hivyo Arsenal na Spurs wanaonekana kutoa jicho zaidi kwa Benteke wakati Chelsea kocha wake Jose Mourinho amesema safu yake ya ushambuliaji anaona imeimarika zaidi na ana imani nayo.
 
 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.