Tuesday, October 8, 2013
Cole atupwa nje ya kikosi England,kuikosa Montenegro Ijumaa
Beki wa kushoto wa England Ashley Cole ataukosa mchezo wa Ijumaa wa kuisaka tiketi ya kombe la dunia dhidi ya Montenegro kutokana na kuumia mbavu.
Beki huyo mwenye miaka 32 aliumia kwenye mchezo ambao timu yake ya Chelsea ilipatan ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Norwich na kocha wa England Roy Hodgson amejaza nafasi hiyo kwa kumuita Kieran Gibbs wa Arsenal.
Cole, ameichezea timu ya taifa mara 105 na ameendelea kubakia kwenye timu yake ya Chelsea kwaajili ya matibabu.
Haijawekwa wazi kama atakuwepo kwenye kikosi kitakachocheza mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Poland October 15.
England inahitaji kushinda mechi zote mbili zitakazopigwa Wembley ili kukata tiketi ya kucheza fainali za kombe la dunia ziatakazofanyika mwakani nchini Brazil.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.