GOLIKIPA Thibaut Courtois amefunguka na kuwaambia Chelsea hayuko tayari kuwa kama tairi ya spea kwam golikipa namba moja wa timu hiyo Petr Cech wakati atakapomaliza mkataba wake wa mkopo huko Atletico Madrid mwakani.
Courtois kwasasa anatumikia msimu wake wa tatu kwenye klabu hiyo ya La Liga baada ya kujiunga na Chelsea akitokea FC Genk kwa dau la paundi milioni 7 mwaka 2011.
Thibaut Courtois |
Cech, 31, ambaye amekuwa golikipa chaguo la kwanza la Chelsea tokea alipojiunga akitokea Rennes kwa dau la paundi milioni 7 mwaka 2004,amesaini mkataba wa miaka mingine mine ya kuitumikia Chelsea mwaka 2012.
Peter Cech akifanya yake |
Anasema anajisikia safi akiwa na Atletico ikimfanya kucheza Champions League na anajiona amekua na hasa msimu uliopita ambao wamepata taji la European Super Cup na Copa del Rey.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.