Wednesday, October 16, 2013

Pepe Reina aipotezea Barcelona

Golikipa wa Liverpool anayecheza kwa mkopo Napoli ya Italia Pepe Reina ,31,amekataa kuwa katika mipango ya kujiunga na Barcelona ya Hispania.

Kipa huyo amekuwa akihusishwa kutaka kutimkia kwenye timu hiyo kwenda kuchukua nafasi ya Victor Valdes,anayemaliza mkataba wake lakini yeye amesisitiza kuwa amejikita kwenye kazi yake akiwa na Napoli.

Reina amesema ni kawaida kwa mchezaji kuota kuchezea Barcelona au Real Madrid kwasababu ni timu zenye historia na zenye sifa kubwa lakini hana mawasiliano yoyote na Barcelona,na hayo ni mambo ya magazeti tu.

Anasema ana mkataba na Liverpool mpaka 2016 hajali habari za uvumi,anajisikia fahari kuwepo Napoli na wanajaribu kushinda kitu.

Reina alicheza na Valdes kwenye Academy ya Barcelona.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.