Kamati ya Rufani ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imekutana Jumapili Oktoba 13 kusikiliza maombi ya mapitio na mwongozo ya uamuzi wa Kamati ya Maadili.
Sekretarieti ya TFF iliwasilisha maombi ya mapitio kwa Kamati hiyo ya juu kabisa ya masuala ya maadili kutokana na ugumu wa utekelezaji wa uamuzi wa Kamati ya Maadili juu ya mashauri nane yaliyowasilishwa mbele yake.
Kamati ya Rufani ya Maadili inaendelea na kikao chake leo Oktoba 15 na baadaye itakutana na waandishi wa habari saa 10 jioni kwa ajili ya kutangaza uamuzi wake juu ya mwongozo ulioombwa na Sekretarieti ya TFF.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.