Thursday, October 3, 2013

Kibaden ainanga elimu ya wachezaji wa kibongo,awaponda kushinda kwenye facebook,adai hawajitambui


Na Fatma Abdallah Chikawe
Kocha wa Wekundu wa Msimbazi Simba Abdallah Kibaden amewananga wachezaji wa kibongo akisema wengi hawana elimu na hawajitambui.

Kibaden amesema ni ngumu kuwafundisha wachezaji wa kibongo kwasababu wengi ni darasa la saba na wamekuwa na mambo mengi ambayo yanawarudisha nyuma.

Amesema wachezaji wengi wamekuwa wagumu kuwaelewa makocha sababu ya kutojitambua kwao kiasi cha kuwapa tabu makocha.

Msukuma ndinga huyo wa zamani anasema wachezaji wa kibongo wanashindwa hata kufuata ushauri wanaopewa na makocha kwasababu hawajitambui na hawajui wanataka nini ndio maana wamekuwa hawafanikiwi kwa kiasi kikubwa.

Anasema moja ya mambo ambayo mchezaji anatakiwa kuyazingatia ni pamoja na kujitunza binafsi na hata kuzingatia ratiba ya kupumzika na kulala mapema lakini wamekuwa wanashinda kwenye mitandao ya kijamii mpaka saa 8 za usiku,kitu kinjachowafanya waamke wakiwa wamejichokea.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.