Tuesday, October 22, 2013

Siri ya ugomvi wa Ferguson na Beckham mke ndio chanzo

Sir Alex Ferguson amesema David Beckham ilibidi aondoke Manchester United kwasababu nahodha huyo wa zamani wa England alijifikiria kuwa ni mkubwa zaidi ya kocha huyo wa United lakini pia aliponzwa na mapenzi.

Kwenye kitabu chake alichozindua ,Ferguson amesema alitibuana na Beckham baada ya kuponda kiwango chake kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Arsenal mwaka 2003 kiasi cha kumpiga na kiatu wakiwa vyumbani.
Beckham baada ya kuchapwa kiatu na kibabu Fergie
Ferguson anasema pia alitazama umaarufu wake na style yake ya maisha baada ya mchezaji huyo kumuoa mwimbaji wa POP kutoka kundi la Spice Girls Victoria Adams maarufu Posh.
Posh
Anasema kiungo huyo ndiye mchezaji pekee aliyekuwa chini yake aliyechagua kuwa maarufu,ambaye aliamua mambo yake nje ya uwanja,na yote baada ya kuangukia kwenye mapenzi ya Victoria ndio kulimbadili kila kitu.
Lakini akamsifia Beckham kwa mchango wake kwenye timu ya Manchester United na akisema ni nembo kwa kila mtoto duniani.

Beckham, ambaye alishinda mataji 6 ya ligi kuu Englandmataji mawili ya FA Cup na moja la Champions League akiwa na United aliuzwa Real Madrid kwa dau la paundi milioni 25 mwaka 2003,kabla ya kutimkia Marekani kwenye timu ya LA Galaxy.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.